1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Ukiukaji wa haki za binadamu umeongezeka

27 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3p

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vimeongezeka sana nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika miezi ya nyuma.Ripoti ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Kongo iliyotolewa siku tano kabla ya kufanywa chaguzi za rais na bunge nchini humo, imesema kuwa vitendo vingi vya kisiasa vilivyokwenda kinyume na haki za binadamu vimeshuhudiwa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2006.Tume ya Umoja wa Mataifa imekosoa polisi,idara ya upelelezi na wana jeshi waliotumia nguvu kuyavunja maandamano ya kisiasa. Jumapili ijayo,raia wanapiga kura kumchagua rais na bunge jipya.Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu miaka 40 unaoruhusu zaidi ya chama kimoja kushiriki.