1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Kikosi cha Umoja wa Mataifa kimeua waasi huko Ituri

2 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFaJ

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko nchini Kongo-Kinshasa wamewaua zaidi ya wanamgabo 50 wa vikosi vya waasi, wakati wa mapigano.

Kwa mujibu wa maelezo ya kikosi cha kulinda amani nchini Kongo, mapigano haya yalitokea baada ya wanajeshi wa umoja wa mataifa kuanza msako kwenye eneo la Ituri huko kaskazini-mashariki mwa nchi.

Ijumaa iliyopita, wanamgambo hao wa waasi walivamia eneo hilo la kuwaua wanajeshi 9 wa Umoja wa Mataifa.