1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Maelfu wakimbia kushtakiwa na mahkama za Gachacha

24 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJr

Maelfu ya wananchi wa Rwanda wamekimbilia nchi ya jirani ya Uganda na Burundi kwa kuhofia kushtakiwa na mahkama za kienyeji za Gacaca zinazoendesha kesi dhidi ya Wahutu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Waziri wa serikali za mitaa Protais Musoni ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba watu wanaofikia 2,000 wamekimbilia Burundi na wengine 1,200 wamekimbilia Uganda kwa kuhofia kutotondewa haki na mahkama hizo za jadi za Gacaca.

Waziri huyo ameseme wana ripoti ya idadi kubwa ya watu wanaokimbia na wamelifikisha suala hilo kwa serikali ya Burundi na Uganda na kwamba wanaandaa mipango ya kuwarudisha watu hao.