1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mji wa Kiev washambuliwa tena na Urusi

1 Juni 2023

Maafisa wa Ukraine wamesema kuwa mashambulizi ya makombora ya Urusi usiku wa kuamkia leo yameuawa watu watatu, wawili wakiwa ni watoto.

https://p.dw.com/p/4S38b
Ukraine Krieg | Raketenangriff auf Kiew
Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Watu wengine 14 wameripotiwa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo, ambayo ni ya 18 kuulenga mji mkuu huo wa Ukraine mnamo mwezi Mei.

Meya wa Kiev Vitali Klitschko  amesema jengo la makaazi ya watu pamoja na kituo cha afya vimeharibiwa. Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amearifu kuwa amekwenda nchini Moldova kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya, ambako anatarajiwa kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi kadhaa wa mataifa ya Ulaya.

Katika mazungumzo hayo, amesema ataomba msaada wa ndege za kivita zitakazoisaidia nchi yake kukabliana na mashambulizi ya Urusi.