1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Watu watano wauawa katika shambulizi nchini Ukraine

31 Mei 2023

Takribani watu watano wameuawa na wengine 19 wamejeruhiwa kwa mashambulizi yaliyotokea usiku wa kuamkia leo kwenye jimbo la Lugansk, Ukraine.

https://p.dw.com/p/4S0MV
Moshi ukionekana baada ya shambulizi kwenye mji wa Lugansk, 12.03.2023. Taarifa zilisema, shambulizi hilo lilifanyika kwenye eneo la kiwanda.
Mzozo baina ya Urusi na Ukraine unazidi kuongezeka na hasa wakati huu ambapo mataifa hayo mawili yanaendelea kushambuliana na makombora. Picha: Vladimir Ivanov/TASS/IMAGO

Hayo yameelezwa na maafisa wa usalama wa Urusikatika jimbo hilo, na wamelilaumu jeshi la Ukraine kuhusika na shambulizi hilo. Hata hivyo, maafisa hao hawakuelezea iwapo waliouawa na kujeruhiwa ni raia au wanajeshi. Wamesema Ukraine ilifyatua makombora manne kutoka kwenye moja ya mifumo ya kisasa ya kurushia makombora aina ya HIMARS, ambayo Kiev ilipewa na Marekani. Wakati huo huo, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev, amesema Uingereza ni ''adui wa kudumu'' wa Urusi na kwamba maafisa wowote wa Uingereza waliowezesha vita nchini Ukraine huenda wakachukuliwa kama walengwa halali wa kijeshi. Amesema Uingereza inafanya kazi kama mshirika wa Ukraine kwa kuipatia msaada wa kijeshi unaojumuisha vifaa na wataalamu.