1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM. Msako wafanywa katika kambi za wakimbizi nchini Sudan.

25 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAP

Maelfu ya askari polisi waliojihami kwa silaha pamoja na wanajeshi wamefanya msako katika kambi kubwa za wakimbizi yapata kilomita 30 kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Wanajeshi wasiopungua 6,000 na askari 400 walilizingira eneo hilo, na kuwatia nguvuni watu 50 wanaotuhumiwa kuwauwa askari 17 katika machafuko ya juma lililopita. Watuhumiwa wengine 32 walikamatwa kwa makosa ya uporaji mali na kukikochoma moto kituo cha polisi.

Kambi za wakimbizi na maeneo ya madongo poromoka yanayopakana na mji wa Khartoum ni makazi ya watu zaidi ya milioni mbili, wengi wao wakiwa ni raia kutoka eneo la kusini waliolazimika kuyahama makazi yao kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.