1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khan, ashutumu jeshi kutaka kusambaratisha chama chake

Hawa Bihoga
4 Juni 2023

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan, ameshutumu jeshi na idara yake ya ujasusi kujaribu kukiharibu chama chake cha kisiasa, na kusema "hana shaka" atashtakiwa katika mahakama ya kijeshi na kuswekwa gerezani.

https://p.dw.com/p/4SAgr
Pakistan Ministerpräsident Imran Khan
Picha: K. M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Khan ameyasema hayo katika mahojiano nyumbani kwake na shirika la habari la Reuters na kuongeza kwamba, jeshi limeonesha makucha yake wazi bila kujificha.

Jeshi ambalo limeendesha nchi kwa njia ya moja kwa moja na isyo ya moja kwa moja halijatoa kauli yoyote kufuatia shutuma za Imran Khan.

Soma pia:Rais wa chama cha Imran Khan wa Pakistan atiwa mbaroni

Mvutano wa mwaka mzima kati ya Khan, kiongozi maarufu zaidi kulingana na kura za maoni na jeshi, umechochea machafuko ya kisiasa na kuongeza hali ya sintofahamu katika taifa hilo lenye silaha za nyuklia ambalo pia linakabiliwa na mgogoro wa kichumi.

Pakistan inakibiliwa na mfumuko wa bei na kuporomoka thamani ya sarafu ya nchi hiyo.