1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Imran Khan aachiliwa kwa shtaka jipya la kuchochea ghasia

30 Mei 2023

Waziri Mkuu wa Zamani wa Pakistani Imran Khan leo amepatiwa dhamana kuhusiana na mashtaka mapya ya kuchochea vurugu za wafuwasi wake dhidi ya jeshi baada ya kukamatwa na kuzuiliwa Mei 9 kufuatia kesi ya rushwa.

https://p.dw.com/p/4Ryct
Pakistan Ministerpräsident Imran Khan
Picha: K. M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Wakili wake, Intezar Hussain Punjotha, amesema mahakama inayosikiliza kesi za ugaidi imethibisha dhamana hiyo baada ya kutimiza masharti muhimu ya hatua hiyo.

Kukamatwa kwa Khan Mei 9 kulisababisha maandamano makubwa ambapo wafuasi wake walioharibu majengo na vifaa vingine vya jeshi, hatua ambayo ilizusha hofu ya usalama kwa taifa hilo lenye silaha za nyuklia, ambalo pia linapambana na mzozo wake mbaya zaidi wa kiuchumi uliodumu kwa miongo kadhaa.