1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yabadili hukumu ya kifo kuwa kifungo cha maisha

Thelma Mwadzaya25 Julai 2023

Wafungwa waliohukumiwa kifo nchini Kenya sasa wanashusha pumzi baada ya serikali kutangaza kuwa hukumu hiyo itabadilika kuwa kifungo cha maisha. Amri hiyo inahusu waliohukumiwa kabla ya Novemba mwaka 2022.

https://p.dw.com/p/4UMYy
Kenias Präsident William Ruto
Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Itakumbukwa kuwa hukumu ya kifo ilitekelezwa kwa mara ya mwisho mwaka 1987 baada ya jaribio la 1982 kuipindua serikali ya Kenya.

Kupitia gazeti rasmi la serikali, Rais William Rutoamebadili hukumu za kifo kuwa kifungo cha maisha. Uamuzi huo umepitishwa baada ya kupata ushauri wa kamati ya msamaha ya rais.

Kulingana na mwanasheria mkuu, Justin Muturi, amri hiyo inawahusu wafungwa waliohukumiwa kabla ya tarehe 21 mwezi Novemba mwaka 2022. Jee, hili litaleta afueni ipi kwa wafungwa waliotekeleza makosa mazito?

Soma pia:Amnesty: Idadi ya watu walionyongwa iliongezeka mwaka 2022

Teresa Njoroge ni afisa mkuu mtendaji wa shirika la Clean Start linalowasaidia wafungwa kuanza maisha mapya baada ya kutumikiahukumu zao jela amesisitiza kwamba haki ya maisha ni haki ya kila mmoja na mamalaka zinapaswa kulinda haki hiyo.

"Huku hii inatekelezwa zaidi dhidi ya wanyonge." Alisema na kuongeza kwamba hukumu hiyo inadhalilisha utu wa mtu.

Agizo la Rais limezingatia katiba ya Kenya?

Agizo la rais William Ruto linaendana na ibara ya 133 ya katiba ya Kenya ambayo pia inampa mamlaka ya kutoa msamaha wa moja kwa moja au masharti kwa aliyehukumiwa adhabu yoyote.

Kenia wartet mit Spannung auf das Urteil des Obersten Gerichtshofs zu den Wahlen
Mahakama ya juu ya Kenya ikiendesha shauriPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Itakumbukwa kuwa hukumu ya kifo ilitekelezwa kwa mara ya mwisho mwaka 1987 kufuatia jaribio la kuipindua serikali la 1982. Hezekiah Ochuka alinyongwa kwa kosa la uhaini.

Takwimu zinaashiria kuwa mwishoni mwa mwaka 2021, watu 601 walikuwa wamehukumiwa kifo na hukumu nyengine 14 za kifo zilitolewa mwaka huohuo.

Soma pia:Mahakama ya DRC yawahukumu kifo watu 51 kwa mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa

Wesley Waku ni afisa wa sheria katika shirika la Justice Defenders linalowasaidia wafungwa kueleaw mfumo wa sheria na haki, ansema wengi waliohukumiwa adhabu hiyo hupewa nafasi ya kurekebisha mienendo yao kwenye jamii.

"Dhamira ya haki ni kuruhusu kutoa nafasi nyingine ya kujirekebisha." Alisisitiza katika mtazamo wake.

Ifahamike kuwa bunge la taifa limejitahidi kuifutilia mbali adhabuya kifo bila mafanikio. Miswada iliyowasilishwa mwaka 2007 na 2015 iliangushwa na wabunge waliodai kuwa umma unaiunga mkono.

Tathmini ya mwaka 2021 iliyofanywa na shirika la Death Penalty Project la kutetea haki za wafungwa kwa ushirikiano na tume ya haki za binadamu, KNHCR, ilibaini kuwa wakenya wamegawika nusu kwa nusu mintarafu utekelezaji wa hukumu ya kifo.

Mwaka 2017, mahakama ya juu , iliharamisha hukumu ya kifo ya lazima kwa kuwa inakiuka katiba. Kenya ni moja ya mataifa 17 barani Afrika ambayo hayajatekeleza hukumu ya kifo katika muongo mmoja uliopita.

Hukumu ya kifo hutolewa kwa makosa ya mauaji, yanayosababisha mauaji, wizi na uhaini.

Idadi ya adhabu ya kifo yapungua