1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliohusika na mauaji ya balozi wa Italia DRC wahukumiwa

7 Aprili 2023

Mahakama ya kijeshi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kinshasa imewahukumu siku ya Ijumaa wanaume sita kifungo cha maisha jela kwa kumuua balozi wa Italia mwaka 2021.

https://p.dw.com/p/4PozM
Italienischen Botschafters im Kongo, Luca Attanasio
Picha: AFP/Italy's Foreign Ministry

Balozi Luca Attanasio aliuawa wakati msafara wa Umoja wa Mataifa ulipovamiwa katika eneo la mashariki  mwa nchi hiyo lenye machafuko. Wengine waliofariki kunako tukio hilo ni dereva Mustapha Milambo na afisa wa polisi wa Italia Vittorio Lacovacci.

Soma pia: Polisi Congo yawatia mbaroni washukiwa wa mauaji ya balozi wa Italia

Awali, waendesha mashtaka waliomba hukumu ya kifo kwa washtakiwa hao na kuwaita wanachama wa genge la uhalifu. Washtakiwa hao ambao walikamatwa Januari mwaka jana, walikana mashtaka hayo huku mawakili wao wakisema watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.