1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Polisi yapiga marufuku maandamano mapya ya upinzani

26 Machi 2023

Mkuu wa polisi nchini Kenya Inspekta Jenerali Japhet Koome ametangaza leo kupiga marufuku maandamano ya upinzani yaliyoitishwa Jumatatu, baada ya maandamano ya wiki iliyopita kuzua ghasia na kusababisha vifo.

https://p.dw.com/p/4PGYk
Kenia l Proteste in Nairobi l Ausschreitungen mit der Polizei
Picha: Brian Inganga/AP/picture alliance

Inspekta Koome amewaambia waandishi wa habari kuwa hawaruhusu maandamano yenye vurugu na kwamba maandamano yaliyopangwa kufanyika kesho ni kinyume cha sheria na hayataruhusiwa.

Kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga amewataka watu kuandamana siku ya Jumatatu na Alhamisi ili kupinga hali ya kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya.

Soma pia: Mwanafunzi auawa wakati upinzani Kenya ukifanya maandamano

Katika maandamano ya Jumatatu iliyopita maafisa 31 wa polisi walijeruhiwa huku watu zaidi ya 200 wakikamatwa. Rais William Ruto anayeondoka leo kuelekea barani Ulaya amemtaka Odinga kuachana na azma yake ya maandamano.