1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya iko tayari kupeleka kikosi kuisaidia Haiti

30 Julai 2023

Kenya imesema iko tayari kuongoza kikosi cha kimataifa na itapeleka polisi 1,000 nchini Haiti ili kuisaidia kupambana na magenge ya uhalifu ikiwa nchi hiyo itakubaliwa kufanya hivyo.

https://p.dw.com/p/4UYTt
Polisi wa Haiti wakishika doria kukabiliana na uhalifu
Polisi wa Haiti wakishika doria kukabiliana na uhalifu Picha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya Alfred Mutua ameyasema hayo Jumamosi jioni na kuongeza kuwa maafisa wake wako tayari kutoa mafunzo na kusaidiana na polisi wa Haiti ili kurejesha utulivu.

Soma zaidi: Baraza la usalama la UN lahimiza msaada wa usalama kwa Haiti kukabiliana na magenge

Hata hivyo Mutua amesema pendekezo hilo la kuisaidia Haiti bado linatakiwa kukubaliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa na mamlaka za ndani.

Haiti, imekuwa ikikabiliwa na mizozo ya kiutu, kisiasa na kiusalama huku makundi ya uhalifu yakidhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu Port-au-Prince.

Soma zaidi: Guterres atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuyapa kipaombele mahangaiko ya watu wa Haiti

Mapema mwezi huu, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema  vurugu zimeendelea kupamba moto na kusambaa nchini humo, huku kukiwa na vitendo vya  mauaji, ubakaji, uporaji na maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao.