1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Keir Starmer wa Labour ajiandaa kuiongoza Uingereza

5 Julai 2024

Keir Starmer anajiandaa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya chama chake cha Labour kunyakuwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu.

https://p.dw.com/p/4huDW
Uingereza | Kiongozi wa Labou, Keir Starmer
Kiongozi wa chama cha Labour cha nchini Uingereza Keir Starmer anajiandaa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya chama chake kushinda kwa kishindoPicha: Suzanne Plunkett/REUTERS

Ushindi wa Labour unaufikisha mwisho uongozi wa miaka 14 wa chama cha mrengo wa kulia cha Wahafidhina.

Rishi Sunak amekubali kushindwa kwa chama chake cha Conservative na kumpogeza bwana Keir Starmer na chama cha Labour kwa ushindi wao.

Chama cha Labour kilikusanyika katika sherehe za ushindi wa chama chao mjini London,ambako Starmer mwenye umri wa miaka 61 pamoja na kuahidi  mabadiliko alitahadharisha kwamba kazi haitokuwa rahisi.

 "Siwaahidi mambo yatakuwa rahisi. Kuleta mabadiliko katika nchi sio kitu cha mara moja. Ni kazi ngumu,ikihitaji subira,kujitolea na tutapaswa kuanza kuchukuwa hatua mara moja',' alisema Starmer.

Chama cha Labour kimenyakuwa takriban viti 326, idadi inayopindukia viti vinavyohitajika kupata ushindi mkubwa wa moja kwa moja wa kulidhibiti bunge la Uingereza la viti 650.

Chama cha Conservative kimepoteza viti vyake vingi vilivyonyakuliwa na Labour ikiwemo vilivyokuwa vikishikiliwa na  mawaziri takriban wanane.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW