1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres awataka M23 kuheshimu muda wa kuacha mapigano

Daniel Gakuba
7 Machi 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka waasi wa M23 kuheshimu muda wa kuacha mapigano na kujiondoa kikamilifu katika maeneo waliyoyakamata.

https://p.dw.com/p/4OL40
Katar, Doha | UN LDC5 Konferenz
Picha: Karim Jaafar/AFP/Getty Images

Waasi hao wameyateka maeneo makubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu walipoanzisha upya harakati zao, na kwa sasa wameuzingira mji wa Goma ambao ni makao makuu ya mkoa wa Kivu Kaskazini.

Msemaji wa katibu mkuu huyo, Stephane Dujarric, amesema Guterres pia amelaani vitendo vyote vya vurugu dhidi ya raia, na kuyatolea mwito makundi yote yenye silaha, yawe ya kutoka Kongo au nje ya nchi hiyo, kuweka chini silaha zao bila masharti yoyote.

Kuzuka tena kwa uasi wa M23 kumevuruga vibaya uhusiano baina ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na jirani yake Rwanda, ambayo Kinshasa inaituhumu kuwaunga mkono waasi hao.

Rwanda inazikanusha vikali shutuma hizo.