1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden huenda ikajiunga na Jumuiya ya NATO 2024

2 Januari 2024

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, anatarajia kuwa jumuiya hiyo itaukamilisha mpango wa muda mrefu wa Sweden kujiunga na mfungamano huo wa kijeshi mnamo mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4aoBH
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa NATO, Jens StoltenbergPicha: Government of North Macedonia

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, anatarajia kuwa jumuiya hiyo itaukamilisha mpango wa muda mrefu wa Sweden kujiunga na mfungamano huo wa kijeshi mnamo mwaka huu.

Soma hapa: Sweden yavuka kihunzi kingine uanachama wa Jumuiya ya NATO

Stoltenberg amesema ana uhakika kwamba Sweden itapitishwa kuwa mwanachama wa 32 kwenye mkutano wa kilele wa nchi za NATO utakaofanyika mwezi Julai. Mkuu huyo wa NATO ameliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA, kwamba Sweden imeshatimiza ahadi ilizotoa kwa Uturuki.

Miongoni mwa masharti ya Uturuki ili kuiruhusu Sweden kuingizwa katika jumuiya ya NATO ni kuuziwa ndege za kivita aina ya F16. Ili Sweden iweze kuwa mwanachama wa NATO, wanachama wengine wote wanapaswa kuridhia.