1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaangusha maputo ya Urusi kwenye mji mkuu Kyiv

16 Februari 2023

Ukraine imesema jana kuwa vitengo vyake vya ulinzi wa anga viligundua maputo sita ambayo yanaonekana kutumwa na Urusi kwenye mji mkuu wa Kyiv na kuyadungua mengi yake.

https://p.dw.com/p/4NY4a
Belgien EU und Präsident Selenskyj auf dem EU-Gipfel in Brüssel
Picha: Nicolas Economou/NurPhoto/IMAGO

Maafisa mjini Kyiv walisema maputo hayo yanaweza kubeba vifaa vya uchunguzi na yalitumwa kupeleleza vikosi vyake vya angani.

Uwepo wa maputo hayo angani ulipelekea ving'ora katika mji mkuu wa Ukraine, jambo ambalo kwa kawaida hutokea wakati makombora yanakaribia.

Soma pia:Ukraine yawaomba washirika wa NATO kuharakisha silaha

Mapema siku hiyo msemaji wa Jeshi la anga la Ukraine, Yuriy Ignat, alisema Urusi inatumia maputo "ambayo hayagharimu chochote" ili kuzima makombora ya kudungulia ndege ya Ukraine.

Tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka jana, mamlaka za Ukraine zimeripoti mara kwa mara maputo ya Urusi yanayopeperuka katika anga ya nchi hiyo.