Scholz atarajia mahusiano mazuri na serikali ya Trump
7 Januari 2025Matangazo
Katika mahojiano yaliyochapishwa leo Jumanne na jarida la Stern, Kansela Scholz ametaja dhima muhimu iliyobebwa na Marekani katika maendeleo ya kidemokrasia nchini Ujerumani, katika upande wa Magharibi na kwenye vita vya pili vya dunia na baada ya mapinduzi ya amani upande wa Ujerumani Mashariki.
Soma pia: Kansela Scholz: 'Tunaweza kufanya 2025 kuwa mwaka mzuri'
Scholz amesema msingi huo wa kihistoria unaendelea kuimarisha mahusiano kati ya Ujerumani na Marekani na kwamba ameshazungumza mara mbili na Trump ambaye anaapishwa madarakani tarehe 20 Januari.