1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Kansela Olaf Scholz azungumza na rais wa Kazakhstan

16 Septemba 2024

Kansela Olaf Scholz amefanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na rais wa Kazakhstan

https://p.dw.com/p/4kgmO
Kansela Scholz nchini Kazakhstan
Kansela Scholz akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko ziarani nchini Kazakhstan, ambako amekutana mjini Astana leo na rais Kassym-Jomart Tokayev kuhusu masuala ya ushirikiano wa kiuchumi.

Kansela Scholz ambaye Kazakhstan ni kituo cha pili cha ziara yake ya siku tatu katika eneo hilo la Asia ya Kati, aliyoianzia, Uzbekistan, amesema atafanya kila awezalo kuimarisha uwezekano wa kuwepo mahusiano mazuri ya kiuchumi huku akitowa mwito kwa kuendelea ushirikiano katika sekta ya mali ghafi.

Kazakhstan ni nchi ya tatu msambazaji wa mafuta kwa Ujerumani baada ya Norway na Marekani. Takriban asilimia 11.7 ya petroli ya Ujerumani inatokea katika nchi hiyo yenye nguvu katika kanda ya Asia ya Kati.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW