1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampala. Yoweri Museveni kukutana na Zuma

15 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWf

Rais wa Uganda Bwana Yoweri Kaguta Museveni amekutana leo na makamu wa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma na maafisa wa tume ya uchaguzi ya Burundi ili kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa bunge nchini Burundi unafanyika kama ulivyopangwa.

Afisa wa ngazi ya juu katika wizara ya mambo ya kigeni ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa Bwana zuma, ambaye ni mpatanishi mkuu katika hatua za kuleta amani nchini Burundi , amewasili usiku na kumfahamisha rais Museveni juu maendeleo ya hatua za amani nchini Burundi.

Bwana Museveni ni mwenyekiti wa juhudi za kimkoa za kuleta amani nchini Burundi na mkutano huo unafanyika ili kuweka msisitizo juu ya kufanyika kwa uchaguzi huo , ambao umepangwa kufanyika ifikapo Aprili 22, na kwamba wabunge watamchagua rais mpya na kuunda serikali.

Mwezi uliopita wananchi nchini Burundi walisogea hatua moja zaidi katika kuelekea kuweka mbali miaka 11 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vimeuwa watu zaidi ya 300,000, baada ya kuidhinisha kwa wingi mkubwa katiba mpya inayoelekeza katika kugawana madaraka katika kura ya maoni iliyofanyika nchini humo.