1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Rais Yoweri Museveni wa Uganda, katika risala ...

2 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFn2
yake ya mwaka mpya, amedai majeshi ya serikali yamewashinda vibaya waasi wa chama cha LRA (LORD RESISTANCE ARMY) na amekula kiapo kiongozi wa chama hiki Joseph Kony atauliwa karibuni. Chama LRA kilianza kukamata silaha kuipindua serikali ya Museveni mwaka 1988, ili kuanzisha serikali itakayotegemea misingi ya Maamrisho 10 ya Biblia. Chama LRA kina sifa ovu mno za ukatili na kuwateka nyara watoto wadogo na kimelaaniwa na makundi ya Haki za Binaadam na Mashirika ya Utoaji Misaada ya Umoja wa Mataifa.