1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya maadili ya wabunge wa CCM yawahoji wabunge watatu

Deo Kaji Makomba
3 Septemba 2021

Kamati ya maadili ya wabunge wa chama cha mapinduzi CCM imewahoji wabunge watatu wa chama hicho akiwemo Josephat Gwajima,Jerry Silaa na Hamprey Polepole.

https://p.dw.com/p/3ztHy
Mbunge Josephat Gwajima (kulia) akiwa na mbunge Jerry Silaa (Kushoto) muda mfupi kabla ya kuhojiwa na kamati ya maadili ya wabunge wa CCM mjini Dodoma.
Mbunge Josephat Gwajima (kulia) akiwa na mbunge Jerry Silaa (Kushoto) muda mfupi kabla ya kuhojiwa na kamati ya maadili ya wabunge wa CCM mjini Dodoma.Picha: Deo Kaji Makomba/DW

Kuhojiwa kwa wabunge Josephat Gwajima na Jerry Silaa kunafuatia agizo la bunge la Tanzania kuwapa adhabu ya kuwasimamisha wabunge hao kuhudhuria mikutano miwili ya bunge na kuiagiza kamati ya maadili ya wabunge wa CCM kuwahoji  baada ya kukutwa na hatia ya kusema uongo na kushusha hadhi ya bunge.

Akizungumza mbele ya wandishi wa habari Katika ofisi za makao makuu ya CCM Jijini Dodoma mara baada ya kumaliza kwa mahojiano na wabunge hao, Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya wabunge wa CCM Hassan Mtenga, amesema kuwa kamati yake imewahoji wabunge hao kufuatia agizo la bunge na kuongeza kuwa.

Aidha Mwenyekiti huyo wa kamati ya maadili ya wabunge wa chama cha mapinduzi CCM, ameweka hadharani  sababu ya mbunge wa kuteuliwa wa chama hicho Amphrey Polepole, kuwa amefikishwa katika Kamati hiyo hasa kutokana na kauli zake mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa katika mitandao ya kijamii na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa jamii.

Kamati Kuu ya CCM na hatma ya wabunge

Hassan Mtenga ,mwenye kiti wa kamati ya maadili ya wabunge wa CCM
Hassan Mtenga ,mwenye kiti wa kamati ya maadili ya wabunge wa CCMPicha: Deo Kaji Makomba/DW

Adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya bunge kwa wabunge Josephat Gwajima na Jerry Silaa ilotolewa  hivi karibuni huku Kamati ya Kudumu ya  haki, maadili na madaraka ya bunge ikikielekeza chama cha CCM kuwahoji wabunge hao kutokana tuhuma zinazowakabili.

Mbunge Askofu Josephat Gwajima alifikishwa mbele ya Kamati hizo kufuatia kauli zake kuhusiana na chanjo dhidi ya COVID-19 ambazo amekuwa akizitoa katika kanisa lake la ufufuo na uzima kuwa hazifai huku akiwahimiza waumini wa kanisa lake ulimwenguni kote ikiwemo Tanzania kutokuchanja hadi pale serikali itakapotoa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na usalama wa chanjo hiyo wakati mbunge wa Ukonga Jeryy Silaa akikutwa kosa la kusema uongo ikiwemo kauli yake ya kuwa Wabunge wa Tanzania hawalipi kodi hivyo wanapaswa kulipa kodi kama wafanyavyo wananchi wengine.