1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania : Bunge lawakalia kooni Gwajima na Silaa

Deo Kaji Makomba
31 Agosti 2021

Bunge la Tanzania limetoa maamuzi ya adhabu kwa wabunge wawili wa chama cha mapinduzi CCM, akiwemo Josephat Gwajima kwa kukutwa na hatia ya kusema uongo.

https://p.dw.com/p/3ziz5
Tansania Nationalversammlung 2018
Picha: DW/S. Khamis

Akizungumza bungeni Jijini Dodoma hii leo Mwenyekiti wa Kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge Emmanuel Mwakasaka, amesema kuwa mbunge Josephat Gwajima amekutwa na hatia baada ya Kamati ya maadili kumuhoji juu ya shutuma zinazomkabili na kisha kukiri kuwa maneno aliyoyatoa ni ya kwake mwenyewe na kwamba alikuwa akiwahubiria waumini wake ulimwenguni kote kuhusiana na janga la Covid-19 na chanjo ambazo zinatolewa

Aidha Mwakasaka amesema kuwa kauli za mbunge Josephat Gwajima, zimeleta mpasuko ndani ya nchi hasa wakati huu Tanzania ikikabiliana na mapambano dhidi ya COVID-19 na hivyo kusababisha wananchi kuwa na taharuki hasa wakati huu Tanzania ikiwa imepokea chanjo ya Johnson and Johnson kwa ajili ya kuendesha zoezi la chanjo ambayo ni hiyari kwa watanzania.

Marufuku kushiriki mikutano ya bunge

Gwajima na Silaa wakutwa na hatia ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi ya bunge.
Gwajima na Silaa wakutwa na hatia ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi ya bunge.Picha: Deo Kaji Makomba/DW

Kufuatia kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge kumkuta na hatia mbunge Josephat Gwajima bunge limeazimia kumpatia adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya bunge na kupendekeza kuwa Gwajima ashughulikiwe kwa mujibu wa maadili na afikishwe kwenye chama chake ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia kauli zake.

Wakichangia hoja iliyowasilishwa mezani kwa spika kuhusiana na wabunge Josephat Gwajima na Jery Silaa, wabunge mbalimbali wamesema kuwa Wabunge hao wameonyesha dharau na kiburi hasa wakati walipoitwa mbele ya kamati kuweza kutoa ushahidi na hivyo wanasitaili adhabu

Aidha bunge kwa kauli moja limemtia hatiani mbunge wa Ukonga kupitia CCM Jery Silaa na kumsimamisha kuhudhuria mikutano miwili ya bunge na kushauri aondolewe kwenye uwakilishi wa bunge la Afrika Mashariki kufuatia kukutwa na hatia.  Mbunge Silaa amekutwa na hatia baada ya kutoa kauli kuwa Wabunge katika bunge la Tanzania hawakatwi kodi huku mbunge wa Josephat Gwajima akinukuliwa katika moja ya kauli zake kuwa baadhi ya viongozi nchini Tanzania wamekuwa mlungula ili kuruhusu chanjo kwa Watanzania kitu ambacho Askofu Gwajima alishindwa kuthibitisha.