1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiRwanda

Kagame na Sunak wazungumzia mkataba juu ya wahamiaji

Daniel Gakuba
7 Machi 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amefanya mazungumzo leo na Rais wa Rwanda Paul Kagame kuhusu mpango wa ushirikino baina ya serikali zao kuhusu wahamiaji.

https://p.dw.com/p/4ON8Y
Feierlichkeiten zum Tag der Streitkräfte in Mosambik
Picha: Estácio Valoi/DW

Katika Mpango huo, Rwanda imekubali kuipokea idadi isiyojulikana ya wahamiaji haramu watakaofukuzwa kutoka Uingereza.

Serikali ya London imeutaja ushirikiano kuwa na nia ya kuvunja biashara ya wasafirishaji haramu wa binadamu, wakati huo huo haki za bindamu zikiheshimiwa.

Tangazo la ofisi ya waziri mkuu Sunak limesema yeye na Kagame walizungumza kwa njia ya simu jana jioni, na walikubaliana kuendelea kufanya kazi pamoja kuhakikisha ushirikiano baina yao unatekelezwa kwa ufanisi.

Aidha, kulingana na tangazo hilo, Sunak na Kagame waligusia mzozo unaoendelea mashariki mwa Jymhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na juhudi za kimataifa kuutafutia ufumbuzi wa kudumu.