1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustralia

Sunak na Kishida kusaini mkataba mkubwa wa ulinzi

11 Januari 2023

Waziri wakuu wa Uingereza Rishi Sunak na mwenzake wa Japan Fumio Kishida watasaini mkataba mpya muhimu wa ulinzi utakaowaruhusu wanajeshi wa Uingereza kwenda Japan wakati watakapokutana leo mjini London.

https://p.dw.com/p/4M0PY
COP27 - Rishi Sunak
Picha: Stefan Rousseau/REUTERS

Afisi ya waziri kuu wa Uingereza imesema mkataba huo ni ishara ya hivi karibuni ya kuendelea kuimarika kwa nia na masilahi ya Uingereza katika eneo la Asia Pasifiki, na jitihada za Japan kuimarisha ushirikiano na miungano yake kukabiliana na changamoto kutoka kwa China.

Mkataba huo unaweka msingi wa sheria kwa wanajeshi wa Uingereza na Japan kupelekwa katika pande zote mbili kwa mafunzo na operesheni nyingine.

Sunak na Kishida wanatarajiwa pia kujadiliana kuhusu biashara na uwezekano wa Ujingereza kujiunga na mkataba wa biashara kati ya Australia, Brunei, Canada, Chile, Japan, Malaysia, Mexico, New Zealand, Peru, Singapore na Vietnam.