1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul: Mapigano makali baina ya majeshi ya NATO na Wataliban katika Afghanistan

3 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CBIK

Majeshi ya NATO huko Afghanistan yamesema wanajeshi wao wamewauwa madarzeni ya Wataliban katika siku ya kwanza ya hujuma kubwa mpya katika mkoa wa kusini wa Kandahar. Operesheni hiyo, iliowaingiza wanajeshi 2,000 wa Afghanistan na wale wa NATO, ilifanywa jana. Ndege ya Kiengereza iliokuwa inafanya upelelezi katika eneo hilo ilianguka jana, na kuwauwa wanajeshi wote 14 waliokuwemo ndani yake. Maafisa wa NATO na wale wa Kiengereza walisema ndege hiyo ilikuwa na kasoro za kiufundi na haijashambuliwa kama walivodai Wataliban. Kisa hicho ilikua ni hasara kubwa kabisa ya jeshi la Uengereza katika Afghanistan au Iraq tangu vilipoanzsihwa vita vinavoongozwa na Marekani katika nchi hizo mwaka 2001.