1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kutanuliwa Umoja wa mataifa zaendelea.

Mohammed Abdulrahman18 Julai 2005

Mawaziri nchi za nje wa Ujerumani, Brazil, India na Japan wakutana wa nchi nne wakutana na wenzao wa Umoja wa Afrika kutaka wawaunge mkono, lakini washindwa kuafikiana.

https://p.dw.com/p/CHfr
Waziri wa nje Fischer ambaye nchi yake inawania kiti cha kudumu katika mageuzi ya Umoja wa mataifa.usalama.
Waziri wa nje Fischer ambaye nchi yake inawania kiti cha kudumu katika mageuzi ya Umoja wa mataifa.usalama.Picha: AP

Bila ya uungaji mkono wa Umoja wa Afrika wenye wanachama 53, nchi hizo nne, Ujerumani, Brazil, India na Japan, hazitokua na matumaini makubwa ya kupata theluthi mbili ya kura zinazohitajika au nchi 128 katika baraza kuu la wajumbe 191.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hizo walikutana na mawaziri wenzao kutoka Nigetria, Libya, Afrika kusini na Misri ambazo ni miongoni mwa zinazotajwa kugombea nafasi zitakazotengwa kwa bara la Afrika, huku waziri wa kigeni wa Brazil Celso Amorim akisema masuala yanayofanana baina yao ni makubwa zaidi kuliko tafauti ziliopo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Joschka Fischer alisema baadae kwamba mageuzi yanayotakiwa na anayotaka katibu mkuu Kofi Annan bado yako mbali kwani kwanza lazima yapigiwe kura.

Ujerumani, Brazil, India na Japan zimewasilisha ndizo zilizowasilisha azimio juu ya kutanuliwa kwa baraza la usalama kutoka wanachama 15 hivi sasa hadi 25 , kukiongezwa idadi ya nchi zenye uanachama wa kudumu kutoka 5 hadi 11. Miongoni mwa viti 6 vya kudumu vitakavyoongezwa, viwili ni kwa bara la Asia, viwili kwa Afrika, Ulaya magharibi kiti kimoja zaidi na kimoja kwa Amerika kusini. Kadhalika zimependekeza viti vine zaidi katika mtindo wa kuzunguka miongoni mwa wasio wanachama wa kudumu, ikiwa ni pamoja na kimoja zaidi kwa Afrika.

Lakini Umoja wa Afrika unataka baraza litanuliwe kwa kuwa na jumla ya viti 26. Umependekeza viti 6 vipya vya kudumu pakitengwa viwili kwa bara hilo-na haki ya kura ya turufu. Na katika ongezeko la viti visivyo vya kudumu, Afrika inataka iwe na viti viwili.

Pamoja na hayo kuna mpango wa tatu ambao unapendekezwa kuwa kama ni wa maridhiano. Huo umeandaliwa na mataifa 20 nao unapendekeza viongezwe viti 10 visivyo vya kudumu,huku nchi zitakazoingia ziwe nba vipindi tafauti ili mataifa makubwa yawe na muda wa kutosha. Huo waungaji wake mkono ni pamoja na Kenya, Pakistan, Mexico, Qatar, Uturuki, Uhispania na Korea kusini.

Ufaransa na Uingereza zinaliunga mkono azimio lililoandaliwa na Ujerumani, India, Brazil na Japan, lakini Marekani na China ambazo pia ni wanachama wa kudumu wa Baraza la usalama zinataka mpango wa kulitanua bara hilo ucheleweshwe kidogo.

Baada ya hatua ya kuidhinishwa mfumo muundo wa azimio hilo, itafuata hatua ya pili, ambayo ni kuyapigia kura majina ya nchi zinazogombea. Waziri wa nje wa Ujerumani Joschka Fischer anangali na matumaini akisema “Tunapaswa kuwa kuwastahamilia zaidi marafiki zetu na wengineo, walio na mtazamo mwengine, na kuendelea kubadilishana mawazo.” Baada ya mkutano wao na mawaziri wa nje wa Umoja wa Afrika, walikubaliana kuendelea na majadiliano licha ya kushindwa kuafikiana hapo jana.

Pale zoezi litakapokamilika , itabidi katiba ya umoja wa mataifa ifanyiwe mabadiliko, na hapa kuna wasi wasi kuwa huenda wanachama watano wa kudumu walioko sasa wakatumia kura ya turufu.

Suala la kulitanua baraza la usalama limekua likizungumzwa kwa karibu miaka 12 sasa bila ya kufikiwa suluhisho, hasa kwa sababu kila eneo au nchi ina masilahi na matarajio yake binafsi. Suala hilo lilipata msukumo zaidi mwaka huo pale Katibu mkuu Annan alipohoji kwamba baraza hilo haliwakilishwi ipasavyo na halina budi lirekebishwe kabla ya mkutano wa Viongozi wakuu wa dunia wa Umoja wa mataifa mwezi Septemba.