1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kupunguza wimbi la wahamiaji wa kichini chini barani Ulaya

9 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDE4

Hispania na Senegal zinapanga kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya makundi ya watu wanaoingia kinyume na sheria katika visiwa vya Kanaries.Pande hizi mbili zinapanga kutumia madege kuchunguza mashuwa zinazowasafirisha wakimbizi kabla hazijaondoka Senegal kuelekea mwambao wa Hispania.Hadi hivi sasa nchi hizi mbili zimekua zikishirikiana katika aukaguzi wa baharini ili kuzuwia mikururo ya wakimbizi wanaoingia kichini chini katika visiwa vya Canaries.Wakimbizi 23 elfu wanasemekana wameingia pekee mwaka huu kupitia bahari ya Atlamntik-idadi hiyo ni kubwa mara nne ikilinganishwa na mwaka jana.