1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimbo la Marsabit lathibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa Surua

28 Agosti 2024

Idara ya afya katika jimbo la Marsabit nchini Kenya imethibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa Surua. Jumla ya watu saba wamegundulika kuugua ugonjwa huo katika jimbo hilo la kaskazini mwa Kenya.

https://p.dw.com/p/4k15X
Chanjo ya Surua nchini Tanzania
Chanjo ya Surua nchini TanzaniaPicha: DW

Idara ya afya katika jimbo la Marsabit nchini Kenya imethibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa Surua. Jumla ya watu saba wamegundulika kuugua ugonjwa huo katika jimbo hilo la kaskazini mwa Kenya.

Kuthibitishwa kwa ugonjwa huo katika jimbo hilo, kumewapa wakaazi wasiwasi mkubwa wakati ambapo mamlaka za Kenya zimekuwa mbioni kupambana na kuenea kwa homa ya nyani Mpox.

Waziri wa afya katika serikali ya jimbo la Marsabit Malicha Boru, amesema watu wanne wamegundukika katika mji wa Horr Kaskazini, huku wengine watatu wakithibitishwa katika eneo la Moyale.Watoto wengi duniani hawana kinga dhidi ya ugonjwa wa surua

Waziri huyo katika kikao na wanahabari, amedokeza kwamba, maafisa wa afya ya umma tayari wameelekea katika maeneo yaliyoathirika kwa lengo la kuuhamasisha umma kuhusu jinsi ya kuzuia ugonjwa huo usiwaambukize watu wengine.