1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi la Israel laamuru watu kuondoka vitongoji vya Rafah

2 Julai 2024

Jeshi la Israel hapo jana lilitoa amri mpya ya watu kuondoka katika baadhi ya maeneo ya Khan Younis na Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Amri hiyo imetolewa kufuatia ripoti za maroketi kuvurumushwa kusini mwa Israel.

https://p.dw.com/p/4hl1f
Israel-Palestina- Rafah
Mzozo wa Gaza-RafahPicha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Jeshi la Israel hapo jana lilitoa amri mpya ya watu kuondoka katika baadhi ya maeneo ya Khan Younis na Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Amri hiyo imetolewa kufuatia ripoti za makumi ya maroketi kuvurumushwa kusini mwa Israel kutokea eneo hilo.

Maelfu ya wakimbizi tayari walikuwa wameondoka eneo la kusini mwa Gaza kabla ya operesheni ya Israel iliyokosolewa pakubwa mjini Rafah. Zaidi ya watu milioni 1 walikuwa wametafuta hifadhi katika mji huo wa mpakani baada ya mashambulizi ya Israel katika maeneo mengine ya eneo hilo.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, amesema kwa mara nyingine hiyo inaashiria kuwa hakuna eneo lililo salama ndani ya Ukanda wa Gaza na kwamba juhudi zaidi zinahitajika kuwalinda raia.

Hayo yanajiri wakati Israel ikimwachia mkurugenzi wa hospitali iliyokuwa kubwa zaidi ya Gaza baada ya kumshikilia kwa miezi 7 bila kufunguliwa mashtaka.