1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

UN yahofia usalama wa raia walioko Rafah

10 Februari 2024

Umoja wa Mataifa umesema una wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa maisha ya raia wa mji wa Rafah ulio Ukanda wa Gaza katika wakati Israel inaandaa mpango wa kufanya operesheni ya kijeshi kwenye eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4cFTM
Gaza- Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiratibu uwasilishwaji wa misaada Gaza: 28.11.2023Picha: Ashraf Amra/picture alliance/Anadolu

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres, Stephane Dujarric amesema kile kilicho dhahiri ni kwamba watu hao wanatakiwa kulindwa na kuongeza kuwa wasingependa kuona idadi kubwa ya watu wakilazimishwa kuyahama makaazi yao.

Zaidi ya watu milioni moja wanajihifadhi kwenye mji huo wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wengi wakiwa wamekimbia mashambulizi ya ardhini ya Israel ya Hamas.

Soma pia: Israel yaushambulia mji wa Rafah

Hapo jana ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Misaada ya Kibinaadamu ilisema msongamano mkubwa wa watu katika mji  huo utaongeza ugumu wa kuwalinda iwapo kutakuwa na operesheni ya ardhini.

Inaarifiwa kuwa hata barabara za mji huo zimezibwa kwa mahema yaliyofungwa na familia zinazotafuta eneo tambarare na safi la kuishi.