1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel laendeleza mashambulizi Gaza na Lebanon

8 Oktoba 2024

Jeshi la Israel limesema limeanza mashambulizi dhidi ya kundi la Hizbullah kusini magharibi mwa Lebanon, na kutanua operesheni zake za ardhini baada ya kupeleka wanajeshi zaidi wanaokadiriwa kufikia 15,000.

https://p.dw.com/p/4lWzM
Nakili kiunganishi
Polisi wa Israel katika eneo la mpakani
Maafisa wa polisi wa mpaka wa Israel wakikagua eneo ambapo roketi, iliyorushwa kutoka Lebanon huko Maalot, kaskazini mwa Israel, Oktoba 7.Picha: Avi Ohayon/REUTERS

Kwa upande wake, Hizbullah imesema imevurumisha makombora kadhaa kuelekea kaskazini mwa Israel ambako tahadhari za mashambulizi ya anga zimetolewa katika miji ya Kiryat Shmona, Manara na Kerem Ben Zimra pamoja na miji mingine inayopakana na Lebanon. Jeshi la Israel limeendeleza pia mashambulizi katika Ukanda wa Gaza. Takriban watu 28 wameuawa katika operesheni ya jana usiku ya Israel kwenye kambi ya Al-Bureij huko Gaza. Hayo yakiarifiwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi. ataelekea hivi leo nchini Saudi Arabia na katika nchi nyingine eneo hilo ili kujadiliana kuhusu masuala ya kikanda na kushirikiana ili kukomesha kile alichokiita "uhalifu" wa Israel huko Gaza na Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Raia wa DRC wakikimbia mapigano mashariki mwa nchi hiyo
Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW