Macron: Makubaliano ya kusitisha vita yatekelezwe Lebanon
17 Januari 2025Awali viongozi hao wawili walifanya mkutano wa pamoja na waandisi habari mjini Beirut. Macron yuko ziarani nchini humo katika juhudi za kuunga mkono utawala mpya wa Lebanon.
Katika mkutano huo, Macron amesema ni lazima kuwe na matokeo ya haraka yatakayodumu kwa muda mrefu yanayotokana na makubaliano hayo ya usitishaji vita. Amesema kuna uhitaji wa majeshi ya Israel kujiondoa kabisa Lebanon, na kuwa jeshi la Beirut linapaswa kuwa na mamlaka kamili juu ya silaha zozote. Ameyasema hayo siku kadhaa kabla ya siku ya mwisho ya utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha vita itakayofikiwa Julai 26.
Macron aliwasili Beiruit Ijumaa katika juhudi za kuharakisha kuundwa kwa serikali mpya inayoweza kutekeleza kwa haraka mageuzi na kufungua milango ya kuijenga upya nchi hiyo baada ya vita vya mwaka uliopita kati ya Israel na kundi la Hezbollah. Katika juhudi hizo rais huyo wa Ufaransa amesema nchi yake itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa kusaidia kuijenga upya Lebanon utakaofanyika wiki kadhaa zijazo.
Kabla ya kukutana na mwenzake wa Macron amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa mpito Najib Mikat. Mikati baada ya mkutano huo amewaambia waandishi wa habari baada ya mkutano huo kuwa, "Nimefanya mkutano na Mheshimiwa Rais Macron na tumezungumza kuhusu hali ya sasa na umuhimu wa kuendelea kuiunga mkono Lebanon katika nyanja zote. Tumezungumza pia kuhusu changamoto zinazotukabili kwa sasa. Rais Macron ameonesha kuguswa sana na hali ya Lebanon na ameahidi kuendelea kuiunga mkono serikali mpya."
Macron aonesha nia ya kuzungumza na benki ya dunia kuisaidia Lebanon
Mikati ameongeza kuwa Macron ameonesha dhamira ya kuzungumza na benki ya dunia juu ya namna ya kusaidia katika eneo la kusini mwa nchi hiyo.
Kundi la Hezbollah la nchini humo linaloungwa mkono na Iran lilpambana vikali katika vita dhidi ya Israel kati ya mwezi Septemba na Novemba katika eneo hilo.Lebanon,
Wakati huo huo, Emmanuel Macron ametilia mkazo wito wake wa suluhisho la nchi mbili katika mzozo wa Mashariki ya Kati. Amesisitiza kuwa suluhisho katika mzozo huo ni kutambua uhalali wa haki ya Wapalestina kuwa na nchi ili waweze kuishi kwa amani katika eneo huru, kama Waisraeli walivyo na haki ya kuishi kwa amani nchini mwao.
Katika hatua nyingine, kiongozi huyo wa Ufaransa amesema raia wawili wenye uraia pacha wa Ufaransa na IsraelOfer Kalderon na Ohad Yahalomi ni miongoni mwa mateka wa mwanzo watakaoachiliwa huru baada ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hamas.