1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem: Israel haitalipiza kisasi kwa mashambulio ya Tel Aviv

18 Aprili 2006
https://p.dw.com/p/CBIx

Inaripotiwa kwamba serekali ya Israel imeamuwa kutochuka hatua ya kijeshi dhidi ya Mamlaka ya Wapalastina kufuatia shambulio la jana la kujitolea mhanga lililofanywa mjini Tel Aviv. Hata hivyo, waziri mkuu mteule wa Israel, Ehud Olmert, na baraza lake la mawaziri wanayabebesha dhamana Mamlaka hayo kwa shambulio hilo. Afisa wa cheo cha juu wa Chama cha Hamas amesema Israel ilikuwa ya kulaumiwa kwa kuengezeka hali ya wasiwasi na akamlaumu Rais wa Wapalastina, Mahmoud Abbas, kwa kuyalaani mashambulio hayo. Hii inafuatia lawama nyingi duniani kutokana na hujuma hiyo ambapo watu tisa walikufa na wengine 50 walijeruhiwa.

Japan nayo imesema itasitisha kutoa msaada kwa serekali ya Wapalastina inayoongozwa na Chama cha Hamas hadi pale chama hicho kitapoahidi kuambatana na mwenendo wa amani.