1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jakarta. Waasi waanza kukabidhi silaha.

16 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEal

Waasi wa zamani katika jimbo la Aceh nchini Indonesia wameanza kuzikabidhi silaha zao chini ya makubaliano ya amani yanayosimamiwa na wachunguzi kutoka bara la Asia na Ulaya.

Wanachama wa kundi la harakati za kuikomboa Aceh ama GAM wamekabidhi silaha karibu 90.

Silaha nyingine 800 zitakabidhiwa kabla ya mwisho wa mwaka huu. Mkataba huo wa amani , uliotiwa saini na Finland mwezi uliopita na kundi la GAM na serikali ya Indonesia , una lengo la kumaliza karibu miongo mitatu ya mzozo ambao umechukua maisha ya zaidi ya watu 15,000.

Kwa upande wa Indonesia itapunguza majeshi yake ya usalama kwa nusu katika jimbo hilo la Aceh.

Kiasi cha polisi 1,300 wameondoka katika jimbo hilo siku ya Jumatano. Waandishi wa habari wanasema kuwa makubaliano hayo yameamsha matumaini miongoni mwa wakaazi milioni nne wa eneo hilo la Aceh ambao bado wanaendelea kujikwamua kutokana na maafa ya mwezi Desemba ya Tsunami.

Kwa wachunguzi wa umoja wa Ulaya huo ni ujumbe wao wa kwanza wa kuwanyang’anya silaha wapiganaji katika eneo la bara la Asia.