1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISRAEL YAVAMIA KAMBI YA WAKIMBIZI

23 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFq5
GAZA: Wapalestina 5 wameuawa mapema leo hii,baada ya vikosi vya Israeli kuivamia kambi ya wakimbizi katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.Wengine 20 wamejeruhiwa.Shambulio hilo limetokea saa chache tu baada ya wanamgambo wa Kipalestina kuwafyetulia risasi na kuwauwa maafisa wawili wa Kiisraeli jumatatu jioni katikati ya Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa jeshi la Israel,katika shambulio hilo Wapalestina wawili pia waliuliwa.Sasa idadi ya watu waliopoteza maisha yao tangu uasi wa Wapalestina-Intifada kuanza mwishoni mwa Septemba mwaka 2000 ni 3,663 wengi wao wakiwa ni Wapalestina.