1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yashambulia Gaza, Lebanon na Yemen

21 Julai 2024

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati leo Jumapili kufuatia ghasia mbaya ambapo Israel imeishambulia kwa mabomu Gaza, Lebanon na Yemen.

https://p.dw.com/p/4iYO6
Mlipuko wa Nuseirat ukanda wa Gaza
Mlipuko baada ya shambulizi la anga la Israel kwenye jengo la makazi, huko Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.Picha: Omar Naaman/REUTERS

Hatua hii ni kujibu mashambulizi kutoka kwa makundi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran.

Kulingana na Shirika la ulinzi wa raia la Gaza, Makumi ya watu wameuawa tangu Jumamosi kote katika Ukanda wa Gaza, katika mashambulizi yaliyolenga nyumba katikati mwa maeneo ya Nuseirat na Bureij na watu waliokimbia makazi karibu na kusini mwa Khan Yunis.

Soma pia: Netanyahu akosoa uamuzi wa ICJ ni 'uamuzi wa uwongo

Mashambulizi hayo yamejiri saa chache baada ya Hezbollah na mshirika wake Hamas kusema walishambulia maeneo ya Israel kutoka kusini mwa Lebanon.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant ameonya muendelezo wa operesheni zaidi iwapo Wahuthi wataendelea kuwashambulia.