1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yajiandaa kuwapokea mateka watakaoachiliwa na Hamas

24 Novemba 2023

Israel inajiandaa katika kile ilichosema ni "miujiza" wa kuwapokea mateka 13 kutoka Ukanda wa Gaza huku nayo inapanga kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina wapatao 39.

https://p.dw.com/p/4ZQTf
Israel Tel Aviv 2023 | Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Abir Sultan/AP Photo/picture alliance

Hayo yamewezeshwa chini yamakubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza kutekelezwa leo yanayojumuisha pia uwasilishwaji wa misaada ya kiutu na mafuta huko Gaza.

Soma pia:Mateka 13 wa Isarel na wengine 12 wa Thailand waachiwa na kuruhusiwa kuondoka kutoka kwenyae Ukanda wa Gaza

Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi ambaye nchi yake imesaidia katika kufikiwa kwa makubaliano hayo amesema mpango huu wa kusitisha mapigano kwa siku nne na kutanuliwa mpango huo ili mateka zaidi wanaoshikiliwa na Hamas waweze kuachiliwa huru na pia kuruhusu misaada ambao utawasaidia watu milioni 2.3 ambao wana mahitaji makubwa kuanzia maji, chakula, msaada wa matibabu na kila kitu.


Wakati huo huo Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema mpango huo wa usitishwaji mapigano huko Gaza ni wa muda mfupi tu, na kwamba baadaye nchi yake itaendeleza operesheni yake ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas.