1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendeleza mashambulia yake Gaza

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Jeshi la Israel limeyashambulia tena leo maeneo kadhaa ya yalio chini ya udhibiti wa kundi la Hamas, huku likizidisha operesheni zake za ardhini katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4YALz
Jeshi la Israel israel likiwa katika oparesheni zake za ardhini
Jeshi la Israel israel likiwa katika oparesheni zake za ardhiniPicha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Jeshi hilo limesema ndege za kivita ziliyapiga zaidi ya maeneo 450 ikiwa ni pamoja na vituo vya mawasiliano, uchunguzi, kutolea amri pamoja na vituo vya kurushia makombora.

Taarifa ya jeshi hilo imeongeza kwamba vikosi vyake vya wapiganaji vilishambulia pia vikundi vya kigaidi vilivyojaribu kujibu mashambulizi.

Soma pia:Israel yatanua operesheni ya ardhini Ukanda wa Gaza

Kupitia mtandao wa X, msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema, Israel inaingia katika awamu inayofuata ya vita vyake dhidi ya Hamas huko Gaza kuanzia mashambulizi ya angani, nchi kavu na baharini.

Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas Gaza, imesema hadi sasavifo vya watu ni takriban 7,326 tangu kuzuka kwa vita hivyo mnamo Oktoba 07.