1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD :Wanawake wakaidi kupigwa marufuku kushiriki mbio na wanaume

22 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBV

Mamia ya wanariadha wa Pakistan na wanaharakati wa haki za binaadamu wamekaidi kupigwa marafuku kwa wanaume na wanawake kukimbia bega kwa bega.

Serikali iliahidi kuzuwiya mbio hizo lakini ilikaa pembeni wakati zaidi ya watu 300 wa jinsia zote mbili waliposhiriki kwenye mbio ndefu katika mji wa mashariki wa Lahore.Katika tukio kama hilo wiki moja iliopita polisi ilitembeza mkon’goto kwa wakimbiaji na kuwakamata madarzeni ya watu mara walipoanza kukimbia.

Hata hivyo safari hii polisi wa kutuliza fujo waliwalinda wanariadha hao dhidi ya Waislamu wa siasa kali.Serikali ya mji wa Lahore ilipiga marufuku mbio hizo kufuatia shinikizo kutoka kwa muungano wa vyama vya kidini.

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan amesema mwaka huu watu wanaopinga wanawake kushiriki michezo hadharani wanashauriwa wazizime televisheni zao.