1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yamzika Ebrahim Raisi katika eneo takatifu la Kishia

24 Mei 2024

Iran imemzika Rais Ebrahim Raisi kwenye eneo takatifu zaidi la Kishia nchini humo jana Alhamis, siku kadhaa tangu alipouawa katika ajali ya helikopta.

https://p.dw.com/p/4gDYJ
Iran, Mashhad |Maziko ya Rais Ebrahim Raisi
Raisi na wenzake wamezikwa MashhadPicha: Iranian Presidency Office/AP/picture alliance

Iran imemzika Rais Ebrahim Raisi kwenye eneo takatifu zaidi la Kishia nchini humo jana Alhamis, siku kadhaa tangu alipouawa katika ajali ya helikopta, na kuongezea masaibu ya taifa hilo linalokabiliwa tayari na vikwazo vya kimataifa, machafuko ya ndani na mizozo ya nje.

Soma pia: Tanzia Ibrahim Raisi: Rais mwenye msimamo mkali mwenye ukaribu na Ayatollah Khamenei

Raisi ambaye aliuawa sambamba na waziri wa mambo ya nje na maafisa wengine sita, amezika katika makaburi ya Imam Reza mjini Mashad, ambako Imam wa nane wa Mashia amezikwa, na ambako mamilioni ya mahujaji wa madhehebu hayo hutembelea kila mwaka.

Raisi alikuwa anatarajiwa na wengi kumrithi Ayatollah Ali Khamenei kama kiongozi wa juu wa Iran. Uchaguzi wa kupata mrithi wake umepangwa kufanyika Juni 28.