1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ipo tamaa ya kufanyika mkutano kati ya Trump na Kim Jong Un

31 Mei 2018

Rais wa Marekani Donald Trump amesema wajumbe wa Korea Kaskazini na Marekani wanaohudhuria mkutano huko jijini New York wamepiga hatua nzuri. Waziri Pompeo anakutana na mjumbe wa Korea Kaskazini Kim Yong Chol.

https://p.dw.com/p/2yj9j
Bildkombo Mike Pompeo und Kim Young Chol
Picha: picture-alliance/Yonhapnews Agency

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na afisa mwandamizi wa Korea Kaskazini Kim Yong Chol aliyekuwa afisa wa cheo cha juu wa shirika la ujasusi la Korea Kaskazini katika siku yao ya pili ya mazungumzo wanajaribu kutafuta suluhisho la tofauti zao kati ya kuhusu mpango wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini na kuleta uwezekano wa kufanyika mkutano wa kihistoria kati ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un.

Mikutano kati ya bwana Mike Pompeo waziri wa mambo ya nje wa Marekani na Kim Yong Chol inanaendelea vizuri. Rais Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa kijeshi huko Maryland kwamba viongozi wa Korea Kaskazini wanatarajiwa kesho kwenda mjini Washington na barua kutoka kwa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un. Ikulu ya Marekani imesema maandalizi ya mkutano wa kilele wa Juni 12 yanaendelea pamoja na kuwa rais Trump aliufutilia mbali mkutano huo mnamo tarehe 24 ya mwezi huu wa Mei. Rais Donald Trump amesema waziri wake wa mambo ya nje amekuwa na mikutano yenye tija na kwamba yeye na mjumbe huyo wa Korea Kaskazini wataendelea na mkutano mwingine leo hii Alhamisi.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: picture-alliance/MediaPunch/CNP/C. Kleponis

Marekani inaitaka Korea Kaskazini iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia huku kukiwa na taarifa kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kuzindua kombora lake la nyuklia lenye uwezo wa kuifikia Marekani. Korea Kaskazini kwa muda mrefu imekuwa ikisema kwamba inahitaji silaha za nyuklia kwa sababu ya usalama wake.

Afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani aliwaambia waandishi wa habari wakati Pompeo na Kim Yong Chol walipokuwa wanakutana kwamba Korea ya Kaskazini ni lazima ieleze kile itakachofanya kulingana na mahitaji ya Marekani.

Afisa huyo pia ameeleza kwamba rais Trump anaweza kufanya uamuzi kuhudhuria au kutohudhuria mkutano huo wa kilele iwapo hakutokuwepo na maendeleo yatakayo Chochea kufanyika kwa mkutano jkati ya Trump na Kim Jong Un. China mshirika mkuu wa kibiashara wa Korea Kaskazini imesema inaunga mkono na inahimiza dhamira nzuri kati ya nchi hizo mbili.

Mwandishi Zainab Aziz/RTRE/DPAE

Mhariri:Yusuf Saumu