1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOM: Wakimbizi wa ndani DRC wafikia milioni 6.9

31 Oktoba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema kuongezeka kwa ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kumefanya idadi ya wa wakimbizi wa ndani kufikia milioni 6.9.

https://p.dw.com/p/4YDXT
DR Kongo Weiterhin Kämpfe im Osten | Rusayo IDP Camp
Kambi ya wakimbizi wa ndani huko Rusayo huko GomaPicha: Alexis Huguet/AFP

Shirika hilo limesema Kongo inakabiliwa na mojawapo ya  mgogoro mkubwa zaidi wa kibinaadamu duniani na kwamba kufikia Oktoba 23, takriban watu milioni 5.6 ambao ni wakimbizi wa ndani, walikuwa wakiishi katika majimbo ya mashariki ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Ituri na Tanganyika.

IOM imesema watu hao wanahitaji pakubwa misaada ili kukidhi mahitaji yao ya msingi.

Mgogoro kati ya waasi wa M23 na wanamgambo watiifu kwa serikali ya DRC umeongezeka katika jimbo la mashariki la Kivu Kaskazini tangu mapema mwezi huu hasa kaskazini mwa Goma. Rwanda inashtumiwa kuwaunga mkono waasi hao wa kitutsi wa M23, jambo ambalo Kigali imekua ikilikanusha.