1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SayansiAsia

India yatuma chombo kulifanyia utafiti Jua

2 Septemba 2023

India leo imerusha chombo cha anga za mbali kitakachokwenda kulifanyia utafiti Jua kiasi wiki mbili tangu ilipofanikiwa kutuma chombo kingine mwezini.

https://p.dw.com/p/4VsS0
Chombo cha anga za mbali cha India Aditya L1 kikianza safari ya kwenda kulitafiti jua
Chombo cha anga za mbali cha India Aditya L1 kikianza safari ya kwenda kulitafiti juaPicha: AP

Roketi iliyobeba chombo hicho cha utafiti wa Jua kilichopewa jina la Aditya-L1, iliruka mapema leo alfajiri kuanza safari ya kiasi umbali wa kilometa milioni 1.5 kutoka sayari ya dunia.

Shirika la Utafiti wa Anga za Juu la India limesema chombo hicho kitatafiti tabaka la juu la Jua, maumbile na upepo kwenye nyota hiyo yenye dhima kuu katika mfumo wa sayari unaoijumuisha dunia.

Hatua hiyo inafuatia mafanikio ya mnamo Agosti 23 ambapo India ilikuwa taifa la kwanza duniani kupeleka chombo kwenye ncha ya kusini mwa mwezi. Utafiti kuhusu Jua na mafanikio ya kutuma chombo mwezini kunaimarisha nafasi ya India katika shughuli za utafiti wa anga za juu duniani.