1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiIndia

India yaiomba Marekani kuachia fedha zake dola milioni 26

31 Agosti 2023

India imeiomba Marekani iruhusu kuachiwa kwa dola milioni 26,fedha za makampuni kiasi mawili ya India ya biashara ya almasi.

https://p.dw.com/p/4VnJE
Russland ALROSA Diamantensortierzentrum in Jakutien
Picha: Alexander Ryumin/TASS/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa duru za serikali ya India, Marekani ilizizuia fedha hizo kutokana na makampuni hayo kudaiwa kufanya biashara na Kampuni kubwa ya almasi ya Urusi iliyowekewa vikwazo ya Alrosa

Fedha hizo zilizuiliwa mwanzoni mwa mwaka huu kufuatia vikwazo vya Marekani dhidi ya kampuni hiyo vilivyowekwa Aprili mwaka 2022 na ofisi ya hazina ya  Marekani inayodhibiti mali za kigeni.

soma pia:China yaichokoza India kwa ramani mpya rasmi

Baadhi ya wanachama wa  kundi la nchi tajiri duniani la G7 wametaka vipitishwe vikwazo vikali dhidi ya biashara ya almasi kwa makampuni ya Urusi.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW