1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

India na China kudumisha amani na utulivu kwenye mpaka wao

16 Agosti 2023

Makamanda wa jeshi la China na India wameahidi kudumisha amani na utulivu kwenye mpaka wao unaogombaniwa.

https://p.dw.com/p/4VFDA
Bendera za China na India
Bendera za China na IndiaPicha: Yann Tang/Zoonar/picture alliance

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoonekana kutoka pande zote kutuliza hali baada ya kuongezeka kwa mivutano.

Wizara ya ulinzi ya China imetoa taarifa ya pamoja kwenye mitandao ya kijamii ikisema kuwa mazungumzo ya duru ya 19 ya ngazi ya makamanda kati ya pande hizo mbili yaliyofanywa Jumapili na Jumatatu yalijadili kwa kina namna ya kuyatutua masuala yanayohusiana na udhibiti wa upande wa magharibi wa mpaka wao.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya China Wang Wenbin ameyapongeza mazungumzo hayo leo yaliyofanyika katika kituo cha kijeshi cha India cha Chushul-Moldo, akiongeza kuwa pande zote mbili zitaendeleza mazungumzo kupitia mbinu za kijeshi na kidiplomasia.