1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Imran Khan ahukumiwa miaka 10 jela

31 Januari 2024

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, ikiwa ni chini ya wiki mbili kabla ya nchi hiyo kupiga kura katika uchaguzi ambao chama chake kinazuiwa kushiriki.

https://p.dw.com/p/4brR6
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan na mkewe Bushra Bibi
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan na mkewe Bushra BibiPicha: Arif AliAFP

Hukumu hiyo ya hatia ya kufujisha nyaraka za siri za serikali ilitolewa ndani ya gereza la Adiala, ambako Khan amekuwa akizuiliwa kwa muda mwingi tangu alipokamatwa Agosti.

Pakistan itafanya uchaguzi Alhamisi ijayo katika kura ambayo tayari imekumbwa na madai ya udanganyifu, huku Khan akizuiwa kugombea na chama chake cha Pakistan Tahreek-e-Insaf - PTI kikikumbwa na ukandamizaji mkubwa.

Khan alifungiwa kushiriki kuhusiana na hukumu ya awali ya rushwa, moja ya kesi kadhaa zilizoko mahakamani ambazo anasema zimefunguliwa ili kuzuia kurejea kwake madarakani baada ya kampeni ya kukaidi dhidi ya wakuu wa kijeshi wa Pakistan.