1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Tume ya haki yaonesha wasiwasi wa uchaguzi huru Pakistan

2 Januari 2024

Tume huru ya haki za binadamu ya Pakistan imesema kuna nafasi ndogo ya kufanyika uchaguzi huru na haki wa ubunge katika uchaguizi wa mwezi ujao kwa sababu ya kile walichokiita kuna mpango wa "wizi wa kabla ya uchaguzi."

https://p.dw.com/p/4amIg
Imran Khan
Picha: Mohsin Raza/REUTERS

Kadhalika tume hiyo imeonesha wasiwasi kuhusu mamlaka kuwazuia wagombea wa chama cha  Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan.Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Islamabad, mwenyekiti mwenza wa Tume ya Haki ya Binaadamu ya Pakistani, Munizae Jahangir, amesema pia vyama vingine vya kisiasa vimewekewa mbinu sawa hizo lakini kwa viwango tofauti. Khankwa sasa yuko gerezani anatumikia kifungo cha miaka mitatu baada ya kufikwa na hatia ya rushwa. Pia anakabiliwa na rundo la mashtaka mengine, hali inayoleta ugumu kwake ugombea nafasi ya hiyo.