1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya watu wanaoishi kambini yaongezeka duniani

25 Oktoba 2023

Idadi ya watu wanaolazimika kuishi kambini badala ya majumbani mwao duniani kote imepita milioni 114.

https://p.dw.com/p/4Y1uA
Baadhi ya raia waliokimbia mapigano Sudan wakiwa katika moja ya kambi ilio chini ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR
Baadhi ya raia waliokimbia mapigano Sudan wakiwa katika moja ya kambi iliochini ya shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCRPicha: JOK SOLOMUN/REUTERS

Makadirio hayo yametolewa na Umoja wa Mataifa leo, ukisema ni idadi ya juu zaidi kuwahi shuhudiwa.

Kupitia taarifa, shirika linalowahudumia wakimbizi la Umoja wa MataifaUNHCR, limetaja vita, mateso, machafuko na visa vya ukiukwaji haki za binadamu kote ulimwenguni kuwa vimechangia idadi hiyo iliyojumuisha hadi takwimu za mwisho wa mwezi Septemba.

Soma pia:Kupunguzwa ufadhili kwatishia elimu kwa wakimbizi Rwanda

Msemaji wa UNHCR, amelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba hiyo ndiyo idadi ya juu zaidi shirika lake limewahi kurekodi tangu shirika hilo lilipoanza kukusanya data.