1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kupunguzwa ufadhili kwatishia elimu kwa wakimbizi Rwanda

20 Oktoba 2023

Hatua ya Umoja wa Mataifa kupunguza ufadhili kwa wakimbizi wanaoishi nchini Rwanda inatishia haki ya maelfu ya watoto kupata elimu na mustakabali wao katika jumla ya kambi tano za wakimbizi.

https://p.dw.com/p/4Xomw
Watoto wa wakimbizi wakihudumiwa kwenye kituo cha malezi mjini Kigali, Rwanda.
Watoto wa wakimbizi wakihudumiwa kwenye kituo cha malezi mjini Kigali, Rwanda.Picha: Cyrile Ndegeya/AA/picture alliance

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) lilitangaza kupunguza ufadhili wa chakula, elimu, malazi na huduma za afya mnamo wakati matumaini ya kupata dola milioni 90.5 za ufadhili yakififia.

Soma zaidi: Muswada wenye utata wa Uingereza kutaka kuwazuia wahamiaji wasio na vibali kuingia nchini humo, unatarajiwa kuwa sheria sasa

Msemaji wa UNHCR, Lilly Carlislex, amesema hadi sasa ni dola milioni 33 pekee ndizo zilizopatikana, na kuongeza kuwa shirika hilo haliwezi kutimiza mahitaji yote ya wakimbizi.

Rwanda inawahifadhi wakimbizi 134,519, wengi wao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na mataifa mengine.