1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliokufa baada ya ghorofa kuporomoka Nigeria waongezeka

4 Novemba 2021

Idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuporomoka mjini Lagos Nigeria imeongezeka hadi 36.

https://p.dw.com/p/42aym
Nigeria Gebäudeeinsturz in Lagos
Picha: picture-alliance/AP Photo

Ibrahim Farinloye wa Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa Dharura amesema jana mchana miili mengine 15 imepatikana kwenye eneo la tukio hilo.

Zoezi la uokozi likiwa linaingia siku yake ya nne, matumaini ya wanafamilia na wakazi wa eneo hilo yameanza kupotea.

Hakuna mtu aliyeokolewa chini ya vifusi vya jengo hilo tangu siku ya Jumanne. Watu tisa walliokolewa mapema wakiwa hai na wanatajwa kuwa katika hali nzturi hospitalini.

Jengo hilo lilokuwa na ghorofa 21 liliporomoka siku ya Jumatatu wakati wajenzi wake wakiwa bado katika eneo hilo.

Haijulikani ni watu wangapi ambao bado wamefunikwa na vifusi. Lakini mjenzi mmoja amesema takriban watu 100 walikuwa wameajiriwa kufanya kazi katika jengo hilo wakati lilipoanguka, hivyo watu wengine 55 hawajulikani waliko hadi sasa.